Thursday, June 12, 2008

mkombozi

I've been really enjoying the kids here lately - just hanging out, laughing with them. Here are some photos of the center...

the youngest boys' dorm


my good friends joakim and filimon

elizabeth taught the boys how to make a bread oven out of mud


after about a week of drying, she taught the boys (and the cooks here) how to make bread


this is me and some of the boys who still live on the streets, back in March. I did streetwork (during the day...) on Tuesday, and it was great to see the kids again. Although a few of them seemed high on glue, which made me sad. Still, it was nice to connect with them for an hour or so. Most of them know me pretty well by now, and were pretty psyched to see me.

Friday, June 06, 2008

mbona kitu kigumu sana

Wiki hii nimesikitika sana. Sasa sijui nisemaje..... kwanza nataka wote wajue kwamba sio muhimu kwa wazungu wa kawaida kuelewa maneno haya. Halafu naandika Kiswahili ili wajitolee wenzangu na wabongo tu waelewe... na wengine basi watahangaika tu, mi sijali. Na ninyi wabongo kabisa... basi naomba munisamehe kwa Kiswahili kibaya sana!

Nimekaa Tanzania kwa miaka mitatu. Kila baada ya miezi michache, najikuta tena ninahitaji kuaga mtu mwengine. Siku zingine ni kwa ajili ya kifo cha mtu ambaye niko karibu naye. Kifo cha mtu ndiyo ni kitu kigumu sana katika maisha yangu. Siwezi kukizoea. Bahati nzuri labda ni kwamba zaidi ya Baba Jamila, wengine waliofariki miaka hizi walikuwa sio karibu sana nami. Niliwafahamu na kuwapenda, lakini siwezi kusema kwamba walikuwa kama jamaa au ndugu zangu.

Lakini jamaa zangu wote wapo Marekani na Uingereza. Halafu nilipofika Tanzania, nikaanza kujenga marafiki wa karibu ili wawe kama jamaa kabisa. Mfano mmoja ni Baba Jamila, aliyefariki Desemba 2006. Alikuwa kama baba mdogo wangu. Na mtoto yake, Jamila, bado ni mwanangu na ataendelea kuwa mwanangu mpaka mwisho wa maisha.

Maana yangu hapa ni kusema kwamba watanzania wengi wamewahi kuchukua nafasi katika maisha yangu na kuwa kama familia yangu... na ninawashukuru kwa upendo na msaada wanao nionyesha kila siku nikiwa hapa Tanzania.

Lakini pia naomba kueleza zaidi kuhusu marafiki zangu wa kizungu hapa Tanzania. Nilipofika Tanzania nilikuwa na wazungu wengi sana wa Peace Corps. Na katika miaka hizi tumezoeana sana na kupendana. Pia wapo mavoluntia wengine waliofika miaka 2006 na 2007. Aidha wapo wazungu wengine ambao hawafanyi Peace Corps lakini tumefahamiana sana. Marafiki wote wananisaidia, wananipa moyo, na nimefurahi sana kuwafahamu.

Lakini katika wale wazungu wote, wapo wachache ambao wamekuwa kama jamaa kabisa. Kwa mfano, wapo wengine niliofika nao mwezi wa sita, tarehe 16, mwaka 2005. Ndiyo zamani sana! Kwa miaka mitatu sasa tumeshirikiana siku za furaha na siku zingine za huzuni. Baada ya miaka mengi kutegemeana, ni kitu kigumu sana kuwaaga wakiwa wanaondoka Tanzania.

Juzi ilikuwa siku ya huzini kweli kweli kwa sababu Bomba Mbaya, besti yangu, alirudi Marekani ghafla. Bomba, kwa miaka mitatu sasa, amekuwa kama kaka yangu KABISAAAAAAAA. Siwezi kutaja kila kitu tulichofanya pamoja lakini wote wanaonifahamu wanajua kwamba yeye ndiyo ni mtu muhimu sana kwangu. Aliwahi kunitembelea Newala na hapa Moshi, na mi pia nikamtembelea Njombe kijijini. Pia kwa sikukuu nyingi sana tukapanga kusherekea pamoja (mwaka mpya, july 4th, american thanksgiving, septemberfest, nk). Aidha tukaenda pamoja Amsterdam mwaka 2007, tulipojirusha kidogo.... sana.

Ukweli ni kwamba sio muda mrefu sana mpaka nitamona tena. Na bila shaka yuko hai kabisa. Vile vile, ninajua kwamba siwezi kulalimika sana. Lakini bado moyo yangu unaumwa! Sijazoea kuishi hapa Tanzania bila msaada yake, upendo yake, ushauri yake, na urafiki yake. Tangu mwaka 2005 amechukua nafasi ya kaka yangu. Amenilinda, amenichekesha, ameniongoza mpaka Bilikana's.....

Mi nitavumilia na nitaendelea kufurahi sana maisha yangu hapa Tanzania. Lakini siku zingine naona ni kitu kigumu sana kuishi hapa kwa sababu watu wengi naowategemea, wataondoka. Nimeanza kuelewa kwamba, nikiendelea kuisha Tanzania, maisha yangu itakuwa hivi hivi. Wengine wataenda kwao, wengine watafariki, na wengine watahama tu sehemu nyingine.

Labda hii ndiyo ni maisha ya mtu mzima. Nilipofika Tanzania nikajisikia bado ni kijana. Siku hizi naona nimebadilika kidogo. Nimekuwa mama na nimeanza kuelewa ugumu wa maisha kwa watu wengi duniani. Na pia nimepata marafiki ambao ninajiskia ni kama ndugu zangu. Nawashukuru mileleni.

(na we bomba... usisahau kiswahili, besti. Maneno yote hapo juu ni kwa ajili yako tu! Usirudi hapa na kiswahili kilichoharibika kibao. nakupenda brother yangu)